Hapo jana usiku Manchester United ilikamilisha uhamisho wa kiungo Maroune Fellaini, pamoja na kukamilisha usajili huo ambao unaonekana kuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo, kwa mtazamo wangu nadhani walikuwa wanahitaji zaidi kumsajili winga kutokana na utamaduni wa timu hiyo kutengeneza mashambulizi mengi kutokea pembeni,
Tangu enzi za kina George Best,David Beckham, Cristiano Ronaldo na Ryan Giggs ambaye mpaka sasa anaendelea kuichezea timu hiyo, Manchester Utd imekuwa ikisifika kwa kuwa na mawinga hodari. nadhani mapungufu makubwa ya Manchester Utd ni kukosekana kwa mawinga hodari katika siku za karibuni,na nadhani lingekuwa jambo la busara kwa David Moyes kama angemsajili winga kabla ya dirisha la usjili kufungwa hapo jana.
Viwango vya mawinga wa Man Utd msimu uliopita vilikuwaje?
Msimu uliopita haukuwa mzuri kwa mawinga watatu wa klabu hiyo ; Ashley Young, Nani na Antonio Valencia:
Michezo
|
Magoli
|
Nafasi zilizotengenezwa
|
Pasi
|
|
Nani
|
11
|
1
|
11
|
2
|
Young
|
19
|
0
|
35
|
3
|
Valencia
|
30
|
1
|
40
|
5
|
Ukiangalia jedwali hapo juu utaona mawinga wote watatu hawakuwa na makali mbele ya lango la timu pinzani,wachezaji wote watatu kwa pamoja walichangia kwa 2.3% ya mabao yaliyofungwa na UNITED msimu uliopita, inasikitisha mchezaji kama Ashley Young alishindwa kufunga walau bao moja huku winga wa Sunderland Adam Johnson akifunga mabao matano.
Siyo tu wachezaji hawa walikuwa na msimu mbaya kwenye sekta ya kupachika mabao,pia hawakuwa na mchango wa kutosha kwenye sekta ya kusaidia wenzao kufunga kwa pamoja wote watatu msimu uliopita walichangia 19.6% ya nafasi za mabao zilizotengenezwa na Manchester United. Kwa upande mwingine wachezaji watatu wa Chelsea Oscar, Eden Hazard na Juan Mata kwa pamoja walitengeneza 47% ya nafasi zilizotengenezwa na Chelsea msimu uliopita.
Kiuhalisia Man Utd ilitegemea mchango mkubwa kutoka kwa hawa mawinga kutokana na utamaduni wa klabu kushambulia mara nyingi kupitia pembeni,kwa mantiki hiyo mawinga hawakuwa na msaada msimu uliopita kutokana na takwimu zilizopo kitu kilichopelekea Sir Alex Ferguson kulazimika wakati mwingine kumchezesha pembeni Danny Welbeck hasa kwenye baadhi ya mechi kubwa,na hicho kilidhihilisha Ferguson kutokuwa na imani kwa hao mawinga wake watatu.
Nini cha Kufanya?
Mazungumzo mengi ya wadau wa soka hasa mashabiki wa Man Utd walikuwa wakisisitiza timu hiyo kumsajili kiungo wa kati lakini sehemu ambayo kweli ilikuwa inahitaji marekebisho ya haraka ni kwenye ni pembeni. Nadhani walishaona hayo mapungufu ndio maana msimu uliopita walipambana kweli kuwasajili Lucas Moura na Eden Hazard lakini mwisho wa siku wachezaji hao walichagua kujiunga na vilabu vingine (labda ni kutokana na wachezaji hao kuhitaji mishahara mikubwa ).
Kwasasa Ashley Young ana umri wa miaka 28 na kusema ukweli hajaonyesha kiwango kukua tangu ajiunge na Man Utd akitokea Aston Villa, pamoja na msimu uliopita kukosa mechi kadhaa kutokana na majeraha lakini bado hajaonyesha cheche zake.
Nani ni mchezaji mwenye kipaji lakini amekuwa na kiwango cha kupanda na kushuka kama homa za vipindi tangia ajiunge na Manchester United.
Valencia ni mchezaji mzuri lakini hana rekodi nzuri ya kufunga mabao na kibaya zaidi ni winga pasee.lakini amekuwa na msaada kwa staili yake ya uchezaji amekuwa akiisaidia sana timu kuwa na balance kwenye upande wa kulia:
Ukiangalia jedwali hapo juu utaona Valencia alivyo na mchango kutokana na aina ya uchezaji wake, amekuwa akiisaidia timu kupanua uwanja hasa kipindi ambacho inahitaji huduma hiyo pamoja na Valencia kuwa na msaada bado kutokana na aina yake ya kiuchezaji timu himuhitaji katika kila mchezo. Uwajibikaji wake unamfanya kuwa na faida kwenye timu kuliko wenzake kina Nani na Young mfano tu msimu uliopita takwimu zinaonyesha alikuwa na msaada mkubwa kwenye ulinzi ambapo79% ya tackles zake alifanikiwa kuipata mipira kutoka kwa wachezaji wa timu pinzani msimu uliopita,huu ulikuwa mchango mkubwa kwa timu kwa jukumu lake akiwa kama winga.
Hitimisho.
Mawinga wa Manchester United wana udhaifu ukilinganisha na idara zingine ndani ya kikosi kitu kilichopelekea wachezaji kama Shinji Kagawa na Danny Welbeck kulazimishwa kucheza pembeni. Mimi nadhani Ashley Young na Luis Nani wanatakiwa kuongeza viwango vyao ingawa kuna kijana mpya Wilfred Zaha amabaye bado hana uzoefu.
Pamoja na Machester Utd kumsajili kiungo hodari Maroune Fellaini lakini mapungufu makubwa yalikuwa kwenye mawinga.fellaini