Tuesday, September 3, 2013

DILISHI MSHINDI WA BBA ASEMA ANA HAMU YA KUMJUA BABA YAKE, SIKU CHACHE KUPITA MKENYA AJITOKEZA NA KUSEMA NI BABA MZAZI WA DILISHI

Wiki iliyopita wakati mshindi wa $ 300,000 za Big Brother The Chase Dillish Mathews kutoka Namibia akifanyiwa mahojiano na mwandishi wa Namibia, alisema anahamu ya kukutana na baba yake mzazi ambaye hawajawahi kuonana.
Dillish Mathews & Abdi Guyo
Baada ya siku chache kupita hatimaye jana (September 2) mwanaume aitwaye Abdi Galgayo Guyo alijitokeza katika ofisi za Standard media Kenya na kudai kuwa yeye ndiye baba mzazi wa Dillish ambaye binti yake anahamu ya kumuona.
 
Guyo alirekodiwa na kituo hicho na kutoa maelezo ya jinsi alivyokutana na mama yake Dillish aitwaye Selma Pashukeni mpaka walivyompata Dillish na baadaye kupotezana.
 
Bwana Guyo ambaye ni askari mstaafu wa Kenya aliiambia Standard Media kuwa alikuwa ni miongoni mwa maaskari wa Kenya wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa mataifa ‘United Nations Transition Assistance Group ‘, kilichopelekwa nchini Namibia kuanzia (April 1989) mpaka (March 1990) kusimamia mchakato wa amani pamoja na uchaguzi wa kwanza wa nchi hiyo na huko ndiko alikutana na Selma.
 
Abdi Guyo, alisema baada ya kukutana na mama yake Dillish Selma walipendana na kumpeleka katika kambi ya jeshi walikofahamiana vizuri zaidi kimapenzi mpaka Selma kubeba ujauzito wa Dillish, Guyo aliongeza kuwa baada ya kurejea Kenya alikuwa akituma barua kwa Selma kabla ya kupoteza mawasiliano.
 
Wiki iliyopita Jumatano, Rinelda Mouton, mwandishi wa habari wa Namibia alifanya mahojiano maalum ambayo Dillish na familia yake walitaka kukutana na baba yake halisi.

 Katika mahojiano hayo Dillish alisema mama yake aliwahi kumwambia kuhusiana na baba yake Mkenya.

Dillish mwenye miaka 22 alizaliwa mwaka 1991.