Mwanamke akamatwa na madawa ya kulevya katika uwanja wetu wa ndege mchana huu
Mama mmoja wa kinigeria amekamatwa na madawa ya kulevya mchana huu katika uwanja wa ndege wa JNIA akijaribu "kum-bypass " Dr.Mwakyembe.
Mwana mama huyo aliyetambuliwa kwa jina la Ojo Athnonie alikuwa amevaa bai bui kwa juu na kufunika sura yake yote.....
Taarifa zinaarifu kwamba mama huyo alikuwa akienda na Ethiopian Airways na hivi sasa yuko chini ya ulinzi mkali wa polisi .....
Kaimu kamanda wa polisi katika uwanja huo, Kamanda Renatus Chalia amesema raia huyo aliingia nchini tangu tarehe 30 mwezi wa nane mwaka huu kama mfanyabiashara wa viatu na mikoba.
Mwanamke huyo anadaiwa kutumia ubunifu wa ziada kwa kanunua powder za johnson kubwa na kuzikata kwa juu na kisha kuweka kete 99 ambazo zote zimenaswa.