Wednesday, August 28, 2013

RAY C KWENDA GYM KWA AJILI YA KURUDISHA NYONGA ZAKE NA KUONDOA MANYAMA


Zaidi ya sauti yake na uwezo mkubwa wa kuimba nyimbo zinazoshikika kiurahisi, umaarufu wake mwingine mkubwa toka enzi hizo ni kiuno bila mfupa kwa jinsi alivyokua akicheza nacho.Huu  ni uwezo uliofanya mpaka maneno ya kiuno bila mfupa yakapata umaarufu kupitia yeye.
 
Siku kadhaa  baada ya kutangaza kurudi kwenye muziki kama zamani, Ray C akiwa ametoka kwenye matibabu ya matumizi ya dawa za kulevya  ameanza kujipanga kupunguza unene alionao ili awe mwepesi zaidi ya alivyo sasa ili kila kitu kiende kama kilivyokua.
 
Ray C akipiga story na fans wake alisema “Mauno ni nyonga si manyama”....hii ni moja ya sababu za msingi sana zilizomfanya Rehema Chalamila kuingia gym kuanza mazoezi.