Jeshi la Polisi Kanda ya Kinondoni limetoa kauri nzito kuhusu picha za udhalilishaji zilinazosambazwa na wasanii wetu wa bongo movie zikiwemo za Manaiki Sanga.
Akiongea katika mahojiano maarumu mkuu wa kituo cha Polisi Oysterbay “OCD” Mtafungwa alisema kuwa kimsingi kupiga picha za utupu ni kosa kisheria hivyo endapo muhusika akimatwa atashtakiwa kwa mujibu wa sheria.
Mtafungwa aliendelea kufafanua kuwa” Unajuwa Jeshi la Polisi lipo kwa ajili ya kusimamia sheria iliyowekwa na serikali hivyo huwa kuna namna ya kuwakamata wahusika hasa kama kumetokea malalamiko toka idara flani kuhusiana na matukio yoyote yanayopelekea uvunjifu wa amani au kupotosha maadili” Alisema Kamanda huyo kipenzi cha watu
Aidha Kamanda huyo aliendelea kufafanua “ Pia Jeshi la polisi linamamlaka ya kumkamata mharifu yeyote kwa muda wowote endapo kipindi hicho akikutwa anafanya uharifu ni pamoja na upigaji picha hizo chafu, Lakini kubwa tuhajitaji kumkata mtu na ushahidi ili iwe rahisi kumbana na kumfikisha mbele ya sheria” Alisema
Mtafungwa alimaliza kusema “ Tunaendelea kufatilia kupita mitandao ya kijamii ili kuona hizo picha zikoje halafu tuhaahidi kuwatolea taarifa hadharani kupita kwa msemaji wa Jeshi la Polisi Kanda ya Kinondoni RPC Wambura ambae kisheria ndiye mwenye mamlaka ya kusema” Alisema Mtafungwa
Aidha waandishi wetu walifanya kazi ya ziada ya kumtafuta Manaiki Sanga ambae kwa sasa amekimbia Jiji na yuko Wilayani Mufindi Mkoa wa Iringa nyumbani kwao ambapo baada ya kubadili namba ya simu lakini jitahada zilizofanyika zilifanikisha kupata namba yake ya simu mpya na msanii huyo aliweza kufunguka mengi.
Manaiki alianza kwa kusema “ Any ways mimi sina la kuongea kama kuchafuka nimeshachafuka na hivi ninavyokwambia nipo nyumbani kwa mke wangu huku Mafinga kwani kuvuja kwa picha zangu za faragha zimenisababishia matatizo makubwa sana hadi mke wangu amenikimbia” Alisema Manaiki
Hata hivyo tulipohitaji kujuwa kuhusu picha zake zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii na kwenye magazeti pendwa zikimuonesha alikawa amekatwa Manaiki alijibu“ Hata mimi nilishangaa kuona taarifa kuwa nimekamatwa kisa picha zangu binafsi za faragha ukweli kwamba sio kweli. Mimi sikukamatwa kwa kosa hilo isipokuwa nilikamatwa huku Iringa siku nilipokuwa natoka huko Dar na walionikamata ni askari wa dolia na baada ya majibizano ya hapa na pale wakanifunga pingu lakini kabla hawajanifikisha kituo cha polisi Mufindi wakaniachia baada ya kuwaomba radhi kwa kosa la kutovaa mkanda wakati naendesha gari langu nikiwa na mdogo wangu wa kiume” Alisema Manaiki
Manaiki aliendelea kueleza siku iliyouata nilishangaa kuona picha zangu kwenye mitandao ya Facebook na Blogs zilinionesha nikiwa nimekamatwa na polisi na hata sijui ni nani alinipiga hizo picha lakini nadhani huenda wakawa askari wenyewe kwa vile siku hiyo ilikuwa usiku mkubwa na hapakuwa na mwananchi yeyote aliyeshuhudia.
Aidha Manaiki alimaliza kusema kuwa “ Kupotea kwa camera yangu ambayo ilikuwa imesheheni picha zangu na wasanii wenzangu zimenighalimu sana kwani nimepata usumbufu mkubwa sana toka ndani ya familia yangu na huku mke wangu akishindwa kunielewa na kukimbia na kuja huku kwao ambapo nimekuja kwa ajili ya kusuruhisha” Na kuongea kuwa alifanya kosa kubwa baada ya kupotelewa na camera yake hakwenda kutoa taarifa polisi kwa vile alikuwa na camera mbili.
Hata hivyo kufuatia taarifa hiyo mastaa wengi wamekuwa tumbo joto kutokana na kuweka picha ningi kwenye mitandao kwa makusudi ili kujiongezea umaarufu hivyo endapo kweli Jeshi hilo litatilia mkazo suala hilo huenda wako watakao hama mji kwa kuhifia kukamatwa.
Aidha Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam Ally M. O. Mlege alisema kuwa Jeshi la Polisi limeongeza ulinzi maalum usionekana kwenye vituo vya mabasi toka nje ya nchi ikiwa na lengo la kuthibiti uingizwaji wa dawa za kulevya baada ya njia ya Airport kuwa ngumu hivyo wanaamini huenda wafanyabishara hao wakabadilisha mfumo huo.