Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk
Joyce Ndalichako amesema baraza lake linajiandaa kutumia teknolojia ya
kompyuta wakati wa kusahihisha maswali ya mitihani ambayo wanafunzi
wanajibu kwa kujieleza.
Kwa sasa teknolojia ya usahihishaji kwa kompyuta
inayotumika nchini ni ile ya kujibu maswali ya kuchagua tu ya`Optical
Mark Reader’ (OMR) iliyoanza kutumika mwaka jana kusahihisha mitihani ya
darasa la saba.
Akizungumza na mwandishi wetu jana wakati wa
Mkutano wa Mabaraza ya Mitihani Afrika (AEAA), unaoendelea mjini hapa,
Dk Ndalichako alisema: “Kwa kuanzia, Necta itafanya majaribio ya
teknolojia hiyo mwakani na ninaamini itaongeza ubora katika
usahihishaji.”
“Kwa kutumia hii teknolojia msahihishaji hawezi
kuona namba ya mwanafunzi, anachoona ni sehemu ya swali anayotakiwa
kusahihisha na jibu lake, akimaliza swali moja jingine linakuja moja kwa
moja,” aliongeza.
Alisema kwa kutumia teknolojia hiyo, mratibu wa
usahihishaji anaweza kuona kazi inayofanywa na msahihishaji yeyote na
hata kuwapima kama atakuwa na wasiwasi wowote.
Alisema Zimbabwe imeanza kutumia teknolojia hiyo aliyosema itasaidia kuongeza ubora katika suala la usahihishaji.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa
ufunguzi wa mkutano huo jana, alisema teknolojia ya OMR imeongeza ubora
wa hali ya juu kwenye mtihani wa darasa la saba pamoja na usahihishaji
wake.
“Watu wanasema kuwa mtihani wa maswali ya kuchagua
ni mrahisi, lakini hii siyo kweli, inatungwa na wataalamu na inalenga
kumpima mtoto katika kila nyanja, ndiyo maana hata mtihani wa darasa la
saba mwaka jana ilibidi Serikali ishushe alama za kwenda kidato cha
kwanza zikawa 70 badala ya 100,” alisema Dk Ndalichako.
Akizungumzia teknolojia hiyo, Naibu Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema wamebaini kuwa zaidi
ya asilimia 80 ya nchi za Afrika zinatumia mfumo wa usahihishaji kwa
OMR.
Alisema baadhi ya nchi zimeanza kusahihisha kwa
kutumia kompyuta hata katika maswali ya kujieleza na kuwataka Watanzania
kuacha kujirudisha nyuma