Sunday, August 25, 2013

JWTZ YATOA UFAFANUZI KUHUSU MWANAJESHI WAKE ALIYETOROKA NA KUKIMBILIA RWANDA


 
JESHI LA wananchi wa Tanzania (JWTZ), limetoa ufafanuzi kwa kusema kuwa askari wake aliyetoroka jeshini Luteni Kanali Coelestine C. Seromba kwa kusema kuwa ni mzaliwa wa Kagera na siyo Rwanda.

Jeshi hilo limevitaka vyombo vya habari kuacha kuripoti taarifa potofu za afisa huyo ambaye alikuwa akikabliwa na tuhuma za makosa ya kijeshi na baadaye akatoweka wakati mchakato wa kumfungulia mashitaka ukiendelea.

Msemaji wa Jeshi hilo Meja Erick Komba Tamba akizungumza na wanahabari Dar es Salaam siku ya Jumamosi, alisema Seromba alitoroka Desemba 17 mwaka jana baada ya kuona kosa lililokuwa linamkabili linaweza kumtia hatiani, hatua ambayo amesema haina madhara kwa jeshi hilo. 



Kwa kuwa Lut. Kan. Seromba alitambua kuwa ametenda kosa na kuamua kutoroka, hatua ambayo ni kinyume cha sheria za JWTZ, ataendelea kutafutwa na akipatikana, atafunguliwa mashitaka kwa kosa la kutoroka JWTZ.