LIJUE JIWE KUBWA LA MAAJABU LILILOPO TANZANIA
Haya ndio maajabu ya Jiwe la Mbuji Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma
Maana ya neno Mbuji ni "Kitu kikubwa"
- Ni jiwe pekee kubwa Mkoani Ruvuma,2.
- Lina vyanzo vingi vya maji chini yake,
- Ni ngumu kulipanda na ukithubutu yatakayokukuta ni juu yako na tayari Mzungu mmoja kapoteza maisha
- Ni ngumu kulizunguka,
- Hutumika kwa matambiko kwa baadhi ya koo,
- Kuna watu maalumu wanaotoa maelekezo kwa yeyote anayetaka kulifikia ama kupanda,
- Ni kivutio kikubwa kwa wageni wachache ambao hutembelea Litembo, Maguu, Hagati nk huko Mbinga,
- Linaheshimika sana na wakazi wanaolizunguka jiwe hilo,
- Sehemu kubwa ya watu wananchi wanaolizunguka hawajawahi kulipanda wala kulisogelea kwa hofu,
- Jina la jiwe hilo ndilo jina la Tarafa ya Mbuji wilayani Mbinga.
Waweza
kwenda mwenyewe ukashuhudie maajabu ya jiwe hili kama ukiwa mtalii wa
ndani na kushuhudia kwa macho yako na kujua zaidi ya maajabu
yanayopatikana katika eneo hilo kwa ujumla