Wenzake hao wenye hasira walimtwanga kwamangumi
na
mateke, wakimshutumu kwa kutokuwa na ushirikiano na “kuharibu soko” hasa
ukizingatia ilikua ni kipindi cha mwisho wa mwezi, ambapo wateja
wamejaa mkwanja na mahitaji ya kununua ngono yameongezeka.
Wakati wakimpa kichapo, walitaka
kumkeketa (kumtahiri mwanamke) kwa kutumia chupa iliyovunjika “ili iwe
funzo” lakini akaokolewa na walinzi wa usiku (wengi wao ni wateja wake)
kabla hajafanyiwa kitendo hicho.
Msuguano ulianza mwezi uliopita
pale msichana huyo mwenye umbo nyororo na la kuvutia alihamia mitaa hiyo
kitu ambacho kiliwakera makahaba wazoefu hapo maana walimuona kama
tishio kutokana na urembo wake.
Kwa mujibu wa dereva wa bodaboda
anayeitwa Peter, kahaba huyo amekua ni kivutio na anayependwa na wengi
kutokana na uzuri wa umbo lake na rangi nyeupe ya ngozi yake. Zaidi ya
“kupunguza bei,” inadaiwa kuwa kahaba huyo pia anatoa “huduma” kwa
mkopo, kitu ambacho wenzie hawafanyi, hivyo kuzidi kuwaaribia biashara
zaidi.
“Kwa kawaida, bei ni kati ya Ksh
100 mpaka Ksh 500 (kama TZ Shs 2,000 mpaka 10,000) inategemeana na
mteja. Lakini “Brownie” anauza kwa hata Kshs 50 (TShs 1,000)” alidai
Peter.
Idadi ya wateja wake ilikua kwa
wingi na kwa kasi, kitu kilichopelekea wivu na chuki kutoka kwa makahaba
wengine, ndipo walipofikia uamuzi wa kufanya njama za kupanga kumpa
kichapo “ili iwe fundisho.”
Makahaba hao walitekeleza lengo hilo pale walipomzingira kwenye kona, gizani akiwa peke yake, na kumshambulia kikatili.
“Kwani unafikiria sisi tutakula
wapi kama utaendelea kujiuza hii bei hasara.” Mmoja wa wanawake hao
alimkaripia kwa sauti ya juu.
Kahaba huyo alipiga mayowe na
kuomba msamaha kutoka kwa wanawake hao wenye hasira wakati
anashambuliwa, ndipo walinzi waliposikia na kukimbilia kumuokoa.
Walinzi hao walipofika, walikaripiwa na makahaba hao wakiambiwa kuwa hiyo ni ishu ya wanawake, na wao haiwahusu.
““Unajua huyu mama huwa
ananipatia kwa mkopo siku ninazokuwa nimechacha hivyo siwezi muacha
auliwe na hawa mikora” alisema mmoja wa walinzi hao wakati wakijaribu
kumuokoa mwanamke huyo.
“Wateja” wake wengine wakaingilia kumuokoa kahaba huyo ambaye alikua ameumizwa vibaya, na kumkimbiza hospitali.
Inaonekana makahaba wazoefu
maeneo hayo wanatawala “ngome” yao na lazima wakatiwe panga na makahaba
wapya, ambao lazima wajitambulishe kabla ya kujiunga kwenye “soko” lao.“Brownie” bado yuko hospitali akipatiwa matibabu huku wateja wake wakimsubiri apone, ili waendelee kupata “huduma” zake kwa bei nafuu, na kwa mkopo.
“Maisha imekuwa ngumu sana na bei ya kila kitu, hata ya hawa wasichana imepanda sana. Tunaomba serikali iingilie kati ,” mmoja wa walinzi hao alilalamika