Sunday, July 28, 2013

NABIII MTUMISHI WA MUNGU APEWA KICHAPO BAAADA YA KUZINI

MWANAMKE anayejulikana kwa jina la Nabii Juliana wa Kanisa la Miracle Assemblies of God, amepigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa kuingilia ndoa ya Mchungaji Richard Kiondo.
 
Tukio hilo la aina yake ambalo lilikusanya umati wa watu, lilitokea hivi karibuni maeneo ya Ukonga Mazizini, jijini Dar ambapo nabii huyo alipigwa hadi kuchaniwa nguo.
 
Akielezea mkasa huo, mtoto wa mchungaji wa kanisa hilo, Christina Kiondo alisema baba yake alikuwa akishirikiana kwa huduma ya kanisa na Nabii Juliana lakini katika ushirika huo anaamini wawili hao walikuwa na uhusiano usiofaa.
 
Alisema kisa cha nabii huyo kupigwa, hivi karibuni mwanamke mmoja alikwenda nyumbani kwa Mchungaji Kiondo na kuwaeleza watoto hao kwamba anamdai baba yao shilingi 40,000, kitu ambacho kiliwashitua sana kwa kuwa baba yao anaishi kwa nabii na pia hawakujua fedha hizo alikopa kwa ajili ya familia gani.
 
Mtoto mkubwa wa mchungaji huyo, alimtuma mdogo wake nyumbani kwa nabii huyo kwa lengo la kwenda kumuita baba yao ili aje kuzungumza na mwanamke huyo.
 
Ilidaiwa kuwa, mtoto huyo alipofika alikutana na nabii na kumwambia amemfuata baba yake lakini alimfukuza.
 
“Baadaye alikuja hapa nyumbani na kuanzisha varangati kitu ambacho hakikukubalika kwa majirani kwani tangu siku nyingi wanajua uhusiano wake wa baba.
 
“Majirani walitoka kwa wingi baada ya kumsikia nabii akitufanyia fujo, walianza kumshushia kipigo mpaka alipokuja kuokolewa na mjumbe wa eneo hili na kupelekwa polisi,” alisema Christina.
 
Akizungumza na mwandishi wetu, mjumbe wa eneo hilo Joseph John ‘Mzee Kasheshe’ alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alikiri kutokea kwa tukio hilo.
 
Kwa upande wake, mke halali wa mchungaji huo ambaye yuko Mbagala kwa matibabu, alisema alizipata taarifa za nabii huyo kupigwa.
 
Aliongeza kuwa tangu zamani mama huyo alikuwa akienda na mumewe nyumbani hapo akidhani kuwa wote ni watumishi wa Mungu hivyo hakuwahi kuwatilia shaka hadi baadaye sana aliponyetishiwa na watu.
Kufuatia kipigo hicho, Nabii Juliana alipofika polisi alitoa malalamiko yake na kufungua kesi yenye kumbukumbu: MAZ/RB/2246/2013 KUHARIBU MALI.