MTANGAZAJI mahiri wa miondoko ya taarab Khadija Shaibu “Dida” leo anatarajia kufunga ndoa.
Dida anayekitumikia kituo cha Times
FM anafikia hatua hiyo baada kuvunjika kwa ndoa yake na Gervas Mbwiga
“G” iliyofungwa mwezi Julai 2011.
Nani anamuoa, muda gani na sehemu gani bado ni siri kubwa.
Swali linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Dida ni je safari hii atajiita Dida wa nani?
Kufuatia ndoa yake ya kwanza na
mfanyabiashara Mohamed Mchopanga ‘Mchops’ Dida akajiita Dida wa Mchops
na baada ya ndoa yake ya pili jina likwa ni Dida wa G.
Tunaitakia kila la kheri ndoa ya Dida