Wajitokeza
kwa wingi katika mapokezi yaliyoanzia uwanja wa ndege wa Mwanza hadi Mjini
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Baraka Kunisaga (DC. Nyamagana) akimpokea Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa (MB-Monduli) alipowasili leo uwanja wa ndege wa Mwanza.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza (RAS) Doroth Mwanyika akisalimiana na Mhe.Lowassa baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwanza anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mery Tesha .
Waziri Mkuu mstaafu Mhe.Lowassa akisalimiana na Shekh Ferej ambaye aliongoza mashekh na viongozi wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza uwanjani hapo kumpokea.
Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza Shekh Mohamed Bara akisalimiana na Waziri Mkuu msataafu Mhe. Edward lowassa uwajna wa ndege leo.
Shekh Hassan Kabete wa JASUTA
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Seleman Mzee alikuwepo kwenye mapokezi na hapa akisalimiana na Mhe. Lowassa
66666
Kada maarufu wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) wa Wilaya ya Busega Dkt. Raphael Chegeni akisalimiana na Mhe. Lowassa.
Mfanyabiashara maarufu wa Mkoani Arusha na Mjumbe wa NEC (CCM-Taifa) Wilaya ya Arumeru Ndg Mathias Manga na mwekezaji mkubwa wa Jiji la Mwanza akisalimiana na Mh.Waziri Mkuu mstaafu (MB) Edward Lowassa .
Mzee maarufu na Kada wa CCM wa siku nyingi Ally Zagamba akisalimiana na rafiki yake Mhe.Lowassa
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akisaini Kitabu cha wageni VIP baada ya kuwasili leo Jijini Mwanza.
Umati wa wanawake wa dini ya kisilam waliokuwa wamejipanga nje ya VIP kusalimiana na Mhe.Lowassa
Mama maarufu wa Jijiji Mwanza Mama Magige akiteta jambo na Mhe. Lowassa baada ya kusalimiana naye.
Wanawake waliojitokeza kumpokea Mhe. Lowassa

NA G. SENGO
WAZIRI Mkuu mstaafu Edward Lowassa leo amelitikisa Jiji la Mwanza baada
ya mamia ya wananchi,viongozi mbalimbali na wamachinga waendesha
pikipiki (Bodaboda) kujitokeza kwa wingi katika mapokezi yaliyoanzia
uwanja wa ndege wa Mwanza hadi Mjini kati.
Mapokezi hayo yaliyoongozwa na viongozi wa serikali,madhehebu ya
dini,wamachinga ambao ni waendesha pikipiki,wafanyabiashara na makada wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) yaliweza kufunika mapokezi ya awali ya leo
asubuhi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyekuwa amewasili Jijini Mwanza
kwa ajili ya kufungua Kongamano na Mkutano wa wadau wa sekta ndogo ya
Pamba unaofanyika jijini hapa.
Baadhi ya wananchi na wakazi wa Jiji hilo walioongozwa na viongozi wa
serikali na Makada mbalimbali wa CCM na Taasisi na Madhehebu ya kidini
walifurika kwa mamia kumpokea na wengi wa wananchi walikuwa pembezoni
mwa barabara kuu ya kutoka uwanja wandege wakimshangilia huku msafara
wake ukiwa na magari zaidi ya 90 na pikipiki zaidi ya 200 zilizopamba
msafara huo.
Waziri mkuu mstaafu huyo leo anataraji kushiriki harambee ya kuchangia
kituo cha redio IQRA Fm cha jiji Mwanza ili kusaidia kuongeza usikivu wa
matangazo yake na kukidhi haja za kujiendesha katika hafla
itakayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest kuanzia majira ya
saa 1:00 usiku kabla ya tukio hilo Lowassa atatembelea ofisi za Umoja wa
Machinga wa jijini Mwanza (SHIUMA) na kisha kuzungumza nao katika
ukumbi wa New Mwanza Hotel majira ya saa 4:00 asubuhi.
Mheshimiwa Lowassa katika harambee hiyo anatarajiwa kuungwa mkono na
baadhi ya wabunge wenzake, makada mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi,
wafanyabiashara, Taasisi na makampuni ili kufanikisha adhma na lengo
lililokusudiwa kutokana na ushawishi alionao na kwa muonekano wa
mapokezi yaliyofanyika uwanja wa ndege imeonyesha Mhe. Lowassa ni
kipenzi cha watu na bado ananguvu ya kukubalika kwa wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya harambee ya kituo
cha radio IQRA ambayo inaongozwa na taasisi ya kiislamu chini ya BAKWATA
mkoa wa Mwanza Shekhe Hassan Kabete alisema maandalizi tayari
yamekamilika kwa asilimia 100 yakichagizwa na kuwasili kwa mgeni rasmi
Lowassa ambaye ni mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha.
“Tunayo matumaini kwamba tutatimiza lengo la kile tunachotaraji
kukusanya kwenye harambee yetu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 400,
ambapo tayari mfuko wetu umekwisha kusanya kiasi cha shilingi milioni
190 hivyo tunataraji lengo litafikiwa nap engine kuvukwa” alisema Shekh
Kabete.