MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrisho Ngassa, ametamka kwamba kuna baadhi ya mechi matokeo yake ni hujuma za wazi.
Ngassa amesema amekuwa akifuatilia mechi mbalimbali za Ligi Kuu Bara
inayoendelea, lakini kuna wakati anaona wazi kuna hujuma kwa baadhi ya
klabu kupanga matokeo ingawa amegoma kuzitaja mechi hizo.
Alisema kuna baadhi ya timu zimekuwa zikishindwa kuonyesha upinzani
halisi ambapo wachezaji wake wamekuwa wakijirahisisha kupoteza mipira
kirahisi hatimaye timu kupoteza mechi.
“Niwe wazi mimi ni mchezaji najua na nawajua wachezaji wenzangu, kuna
baadhi ya timu zimekuwa zikijirahisisha kufungwa kwa uwazi kabisa,
sisi Yanga ni wazi tumekuwa na mechi ngumu hata kama tunashinda,”
alisema.
“Lakini wapo wachezaji wa timu nyingine wanaonekana wazi kabisa
wanajirahisisha kufungwa kitu ambacho kitaharibu utamu wa ligi huku
mwishoni.”
Source: MWANANCHI
Source: MWANANCHI