Mastaa hao ni miongoni mwa wachezaji nane wa Simba na Yanga ambao
wapo sokoni na wanaweza kusaini mkataba na klabu yoyote muda wowote
kuanzia sasa na siku ambazo klabu zao zitawamiliki kihalali hazizidi 30
kuanzia sasa.
Ingawa klabu zao zimekuwa bize kuwania nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, baadhi ya
wachezaji hao wameanza nyodo na kusisitiza kwamba hawatasaini na klabu
hizo mpaka mwisho wa msimu huku ikionekana kama wanataka kutingisha
kiberiti wapewe dau nono.
Uchunguzi wa Mwanaspoti ambao umethibitishwa na wachezaji hao umeonyesha kwamba wachezaji wa Yanga ambao mikataba yao inamalizika mwezi Aprili 19 Ligi ya Bara itakapomalizika ni kipa, Ali Mustapha ‘Barthez’ ambaye habari za uhakika zinaeleza mazungumzo yake ya kurejea Simba yanakwenda vizuri, beki wa pembeni Mbuyu Twite, washambuliaji Didier Kavumbagu na Said Bahanuzi aliyegoma kutolewa kwa mkopo kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu.

Kwa upande wa Simba wachezaji wanne
ambao mikataba yao ipo ukingoni ni viungo, Uhuru Selemani na Ramadhani
Chombo ‘Redondo’, kipa raia wa Ghana Yaw Berko ambao wote hata hivyo
hawajawahi kuwa na uhakika wa namba kwenye kikosi cha kwanza tangu
kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.Mchezaji mwingine ni beki
wa pembeni Haruna Shamte.
Twite amesisitiza kwamba hatosaini mkataba mpya na Yanga mpaka msimu
utakapomalizika huku ikitafsiriwa kwamba anataka kutingisha kiberiti ili
kurekebishiwa baadhi ya vipengele kwenye mkataba wake na amewaambia
marafiki zake wa karibu kwamba hana raha kwa jinsi anavyoishi na vigogo
wa Yanga kwa sasa.
Habari za ndani zinadai kwamba mchezaji huyo amewahi kufanya
mazungumzo na viongozi wa Azam miezi michache iliyopita hivyo ana imani
kwamba huenda wakampa ofa.
Kavumbagu ambaye amekuwa tegemeo kwenye fowadi ya Yanga alisema:
“Bado sijasaini mkataba mwingine wa kuichezea Yanga, mkataba wangu
unamalizika mwishoni mwa msimu huu (Aprili 19), ingawa tayari nimeanza
mazungumzo ya awali ambayo bado hatujafikia muafaka wa kusaini mkataba
mpya.”