Baada ya hivi karibuni kuandikwa habari iliyoeleza kwamba nchini Kenya kuna demu aliyemzimikia ile mbaya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku akiahidi kumpa penzi zito, mpenzi wa msanii huyo Peniel Mwingilwa ‘Penny’ ameibuka na kudai hatishwi na maneno hayo.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Penny ambaye sasa anapika na kupakuwa kwa Diamond alisema anamuamini sana mpenzi wake huyo na kwamba kuhusishwa kwake na mambo ya mademu kila kukicha kunatokana na kazi yake.
“Yatasemwa mengi lakini siwezi kumuacha Diamond, namuamini na najua haya yote yanayotokea ni kwa sababu ya kazi yake kwa hiyo wanaodhani mimi nitayachukua na kuamua kumuacha watasubiri sana, ndiyo kwanza penzi letu linazidi kushamiri,” alisema Penny.