"NIKIFA SIHITAJI KAMATI YOYOTE YA KUENDESHA MSIBA WANGU" KAMA WALIKULA ZA NGWEA, WATASHINDWA NINI KWANGU?". **NAY WA MITEGO
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Ney wa Mitego, ameweka wazi kuwa
ikitokea amefariki dunia hatohitaji kamati kwa ajili ya kuendesha
mipango ya msiba wake, "#kwa kile anachodai kuwa kamati hizo zipo kwa
ajili ya kuvuna pesa".
Hayo aliweka wazi baada kupokea ujumbe
mfupi kwenye simu yake wenye vitisho uliotokana na mashairi alioimba
kwenye single yake mpya ya 'Salaam zao' .
Ujumbe huo wa vitisho
ambao umepokelewa na msanii huyo umekuja mara baada ya msanii huyo
kuachia single yake hiyo ambapo moja ya mashahiri ni juu ya hela za
rambirambi zilizopatikana katika msiba wa msanii Ngwear pamoja na
Kanumba kushindwa kuwafikia walengwa.
Akizungumza na jarida la
Maisha, mara baada ya kutuma ujumbe alioupokea wa vitisho kwenye ukurasa
wake wa 'Instagram', Ney wa Mitego aliweka wazi kuwa amepokea ujumbe wa
vitisho mara baada ya kuachia nyimbo hiyo.
Alisema kuwa amepokea
ujumbe mbalimbali ambazo zipo zinazowataja wahusika moja kwa moja wale
waliohusika kula rambirambi, huku wengine wakimtumia ujumbe wa kumtisha
kwa kile alichokiimba katika nyimbo hiyo.
"Mimi hata ikitokea
nakufa leo sihitaji mtu yeyote wa kuweka kamati ya mazishi yangu
kwani najua kitakachotokea siyo mazishi bali ni kula hela na rambirambi
hizo kushindwa kutimiza malengo kama yalivyokusudiwa" alisema Ney wa
Mitego.
Aliongezea kuwa hawezi kuacha kuimba ukweli hata kama
ataendelea kupokea vitisho.