Sunday, August 4, 2013

DR SLAA ACHAFUA HALI YA HEWA

DR. SLAA AWAUNGA MKONO WAASI WA KONGO ....AMSHANGAA KIKWETE KWA KUMWINGILIA KAGAME


Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli  yake ya  kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake ...



Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo.

Slaa  aliyasema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

“Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani  na hajachukua hatua dhidi ya wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi...


"Alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda  na  badala  yake amempandisha cheo,” alisema Slaa.



Kauli  Dk Slaa imekuja siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kueleza kuwa Tanzania haina mgogoro na nchi ya Rwanda, kutokana na kauli za kejeli na matusi zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa nchi hiyo dhidi yake na Tanzania.  



 Kumezuka sitofahamu ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda, baada ya Rais Kikwete kuitaka Rwanza  imalize  ugomvi  na  waasi  kwa  njia  ya  mazungumzo  ya  amani...

Rais  Kikwete aliutoa  ushauri  huo  wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.

Ushauri huo ulionekana kumchukiza Rais Kagame, anayedaiwa kuhutubia mikutano kadhaa nchini kwake na kutumia lugha ya matusi, kejeli na dhihaka dhidi ya Rais Kikwete na Tanzania.
 
 
Kitendo  cha  Dr  Slaa  kumkingia  kifua  Kagame  kinatia  shaka  uzalendo  wake  na  chama  chake kwa  taifa  hili ...


Sote  tumekuwa  tukishuhudia  matusi  ya  Kagame  dhidi  ya  Tanzania.Iwaje  Rais  Kikwete  aonekane  mbaya  kwa  kumjibu  Kagame, tena  kwa  lugha  ya  kizalendo??



Kagame  amekuwa  akituhumiwa  na  jumuiya  mbalimbali  za  kimataifa  kwa  kutoa  misaada  ya  kivita  kwa  waasi  wa  M23  ambao  wamekuwa  wakiua  raia  na  kuwabaka  wanawake....


Kauli  ya  Dr  Slaa  ina  mambo  mengi  yaliyojificha  na  huenda  yeye  na  chama  chake  ni  wafuasi  wa  karibu  wa  M23   kama  ilivyo  kwa  Kagame.


Kuwa  mpinzani, haimaanishi  ukosoe  kila  kitu.