FEZA KESSY AJIKATIA TAMAA...KURA YAKO INAHITAJIKA ILI ASITOLEWE BIG BROTHER KESHO
Feza Kessy ameonesha kukataa tamaa na uwezekano wa kupona panga la kesho kwenye eviction ya Big Brother Africa.
Wakati akifua nguo zake bafuni, mrembo huyo alipewa kampani na Beverly na Elikem na kuwaambia kuwa haoni dalili kama ataukwepa msumeno wa kesho.
“Hakika, kama nitapona eviction ya Jumapili hii itakuwa ni miujiza tu,” alisema Feza.
“Ni ngumu kwa wapenzi kwenye nyumba hii. Angalia kilichotokea kwa LK4 na Koketso. Wote walitolewa usiki mmoja. Nadhani kitu kile kile kinaenda kutokea kwetu.”