HABARI
ZILIZOUFIKIA MTANDAO HUU HIVI PUNDE ZINASEMA KUWA WATU 13, WAMEFARIKI
DUNIA NA 11 WAMEJERUHIWA KATIKA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA USIKU WA KUAMKIA
LEO KATIKA KIJIJI CHA NGONGWA MKOANI SHINYANGA KWENYE AJALI ILIYOHUSISHA
GARI AINA YA HICE LENYE NAMBA ZA USAJIRI T 756 CHX NA GARI LILILOKUWA
LIMEHARIBIKA LENYE NAMBA ZA USAJILI T 696 AMS.
AKIZUNGUMZA
KWA NJIA YA SIMU KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA SHINYANGA, KIHEMA
KIHEMA, ALISEMA KUWA MIONGONI MWA WATU WALIOFARIKI DUNIA NI PAMOJA NA
DEREVA WA HICE, ILIYOKUWA NA ABIRIA HAO IKITOKEA KAHAMA KUELEKEA
USHIROMBO AMBAYE ALIFARIKI PAPO HAPO, HUKU MAJERUHI WAKIPELEKWA KUPATIWA
HUDUMA YA KWANA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA.