Sunday, August 11, 2013

BASI LA MERIDIAN LAPATA AJALI MBAYA BAGAMOYO

Baadhi ya abiria wakitafuta mizigo yao baada ya basi walilokuwa wakisafiri nalo la Meridian kupata ajali eneo la Mbwewe Bagamoyo.
BASI la Meridian linalofanya safari zake Dar es Salaam na Rombo limepata ajali mbaya eneo la Mbwewe Bagamoyo mkoani Pwani likiwa safarini kuelekea jijini Dar es Salaam likitokea Rombo. Abiria kadhaa wamepoteza maisha katika ajali hiyo japo idadi kamili bado haijafahamaika.