OPARESHENI Fichua Maovu (OFM)
inayoendeshwa na mapaparazi wa Global Publishers inazidi kufichua
‘madudu’ kwenye jamii, safari hii imekutana na machangu ambao
wamecharuka kuendeleza biashara hiyo kwa kisingizio cha kutafuta fedha
za kununulia futari.
‘Askari’ wa OFM, wiki iliyopita
alifanya uchunguzi katika viunga mbalimbali maarufu kwa biashara hiyo na
kukuta machangudoa wakifanya biashara yao kama inavyokuwa katika miezi
ya kawaida.
Maeneo ambayo yalionekana kushamiri
zaidi kwa biashara hiyo ni Barabara ya Mwananyamala Hospitali, American
Chipsi, Makaburi ya Kinondoni, Viwanja vya Leaders Club, Taasisi ya
Moyo, Jolly Club (Masaki), Hospitali ya Agha-Khan, New Maisha Club
(Masaki) na Coco Beach.
Idadi
kubwa ya wadada hao walipohojiwa na paparazi wetu, walisema wanaendelea
na biashara hiyo kwa kuwa ndiyo waliyoizoea kutafutia kipato na
wakiiacha, watakufa kwa njaa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa
Ramadhan.
Ili kujiridhisha kwa data, paparazi
wetu alijifanya mteja na kukutana na machangu wa Makaburi ya Kinondoni
ambao walidai wanapenda waitwe ‘scraper’ au vyuma chakavu pasipo
kufafanua zaidi, bahati mbaya wakashtukia mchezo:
Changudoa: “We kaka mbona
unatuzingua? We ulivyokuja si ulijifanya mteja, kumbe paparazi, sisi
hatuwezi kuacha kujiuza kwa kuwa ndiyo kazi tuliyoizoea, sasa tukikaa
nyumbani tutapata wapi futari?” alihoji mmoja wa machangudoa.
Paparazi: “Hivi ni kweli nyie mnafunga?”
Changudoa:
“Wewe tumia ubongo na maswali yako yanayotia njaa, hata kama sisi
tunafunga au hatufungi tuna watu wanaotutegemea majumbani kwetu
kuwatafutia futari, sasa tusipohangaika itakuwaje?”
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu
waliozungumza na Ijumaa Wikienda, walionesha kukerwa na tabia hiyo na
kulaani vibaya kwani mwezi huu ni maalum kwa ajili ya kumrudia mwenyezi
Mungu na kuacha dhambi.