RAIS OMARI AL BASHIR WA SUDANI ATOROKA NIGERIA BAADA MBINU ZA KUMKAMATA KUVUJA
Rais Omari Al Bashir wa Sudan jana alilazimika kutoroka nchini Nigeria baada ya mikakati ya kumkamata kuvuja..
Rais Bashir aliyekuwa anahudhuria mkutano wa viongozi wa serikali za nchi za Muungano wa Afrika AU, kuhusu afya mjini Abuja amelezimika kuukatisha mkutano huo na kutoroka nchini humo jana Jumatatu kwa hofu ya kukamatwa
Rais huyo ameondoka nchini Nigeria ikiwa ni chini ya masaa 24 tangu awasili Nigeria.
Makundi ya kutetea haki za kibinadam yameishutumu vikali serikali ya Nigeria, kwa kumualika rais wa Sudan, Omal al-Bashir, nchini Nigeria na siku ya jumapili makundi hayo yalilitaka jeshi la nchi hiyo limkamate rais huyo wa Sudan kabla hajaondoka.
Makundi hayo ya kutetea haki za kibinadam yalisema kuwa, ziara ya rais huyo ni dharau kwa wahanga wa mzozo huo unaoendelea katika eneo la Darfur.
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, imetoa kibali cha kukamatwa kwa rais huyo kwa Sudan kwa tuhumu za kuhusika na mauaji ya halaiki.