JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA , BUXTON CHIPETA AFARIKI DUNIA
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba Jaji mstaafu wa Mahakama Kuu Tanzania, Buxton Chipeta amefariki dunia muda mfupi uliopita.
Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia, Jaji Chipeta alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kisukari ambapo ilifikia wakati akalazimika kukatwa vidole kadhaa vya miguuni.
Enzi za uhai wake, Jaji Chipeta aliweza kujijengea heshima katika kazi yake na kufikia kuwa mmoja wa majaji wanaoheshimika mno hapa nchini.
Pia Jaji Chipeta aliwahi kuwa miongoni mwa majaji wa Tume ya kurekebisha Sheria yeye akiongoza kanda ya Dar es Salaam.
Mpekuzi inaungana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao