Friday, July 5, 2013

MTUUMISHI WA MUNGU MASANJA MKANDAMIZAJI KUTOA NENO LA MUNGU JUMAPILI HUKO MAREKANI



Mtumishi wa Mungu Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji) ambaye yuko nchini Marekani kwa ziara maalum, atahudumu kwa waumini wa jiji la Washington DC na vitongoji vyake siku ya kesho (Jumapili 07/07/2013) 
 
Bwana  Mgaya ambaye pia hufahamika kama Mchungaji Mtarajiwa  na ambaye amekuwa akifanya huduma ya uhubiri nchini Tanzania, atahubiri katika ibada ya jumapili katika kanisa la THE WAY OF THE CROSS GOSPEL MINISTRIES katika ibada ya kawaida ya kila jumapili ambayo hufanyika kuanzia saa saba kamili mchana mpaka saa tisa kamili alasiri (1:00pm - 3:00pm)

Hii itakuwa ni huduma ya kwanza nchini Marekani kwa Mtumishi huyu ambaye ni Mchungaji msaidizi katika kanisa la EAGT Mito ya Baraka lililopo Kariakoo jimbo la Temeke jijini Dar Es Salaam likiongozwa na Askofu Bruno Mwakibolwa na ameshafanya huduma katika sehemu mbalimbali nchini Tanzania.