Jijini Mwanza, majambazi yamevamia makao makuu ya polisi na kuiba vielelezo kadhaa ikiwamo begi na laptop. Imeelezwa kwamba majambazi hao walivunja dirisha kisha wakaingia stoo, baada ya kukuta karatasi na zana nyinginezo ambazo hawakuwa na haja nazo walivunja dali na kuingia chumba cha pili.
Baada ya kupekua na kutokuona cha maana kwao, wakatoboa tena dali na kutokea chumba cha tatu ambako walichukua laptop na begi iliyokuwa na vielelezo mbalimbali. Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza ndugu Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akisema wahusika hawajakamatwa.
Naye Kaimu Mkaguzi Mkuu wa kanda amekiri kupokea taarifa ya tukio hilo na kuomba wananchi kushirikiana na maofisa wa polisi kuwabaini wahalifu