HABARI ZIMETUFIKIA PUNDE TU ZINASEMA
MFANYABIASHARA MMOJA MAARUFU NCHINI AMEMWAGIWA KITU KINACHODHANIWA NI
TINDIKALI NA WATU WASIOJULIKANA MAENEO YA MSASANI JIRANI NA KITUO CHA
POLISI CHA OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM.
JINA LA MFANYABIASHARA HUYO BADO HALIJAJULIKANA, NA HATA POLISI BADO
HAWAJAKANUSHA WALA KUTHIBITISHA TUKIO HILO LINALOSEMEKANA LILILOTOKEA
BAADA YA MUDA WA KUFUTURU KUMALIZIKA.
AIDHA, WANAHABARI WETU WAMESHUHUDIA MAGARI KADHAA YA POLISI YAKIWA
KWENYE MAEGESHO YA DUKA MOJA KUBWA LILILOPO MAENEO KARIBU NA OYSTERBAY
POLICE, AMBAKO HAKUNA ALIYETAKA KUSEMA CHOCHOTE, JAPO HABARI ZINASEMA
HAPO NDIPO TUKIO LILIPOTOKEA.
JUHUDI ZA KUMSAKA KAMANDA WA POLISI MKOA WA KINONDONI AMA KAMANDA WA
KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM AFANDE SULEIMAN KOVA ZINAENDELEA. NASI
TUTAWAJULISHA KILA TUTAPOPATA HABARI ZAIDI.