MWANAFUNZI na mwalimu wake katika
sanaa, Irene Uwoya na Lucy Komba wameingia katika bifu zito chanzo
kikidaiwa kuwa ni mwalimu huyo kumzunguka mwanafunzi wake kwa mumewe,
Hamad Ndikumana ‘Katauti’. Lucy ambaye ndiye mwalimu wa Uwoya kisanaa,
imedaiwa kuwa amemzunguka Uwoya kwa mumewe, Ndiku kwa kisingizio cha
kucheza naye filamu iliyofahamika kwa jina la Kwa nini Nisimuoe?
“Kimenuka! Lucy Komba amemhadaa Ndiku, akazuga kuigiza naye filamu moja ndipo walipozama kwenye ukaribu kwelikweli.
“Mbaya zaidi filamu yenyewe wameigiza
wahusika wawili tu (Lucy na Ndiku) mwanzo mwisho kule Tegeta. Sasa wewe
unafikiri kuna nini hapo kama siyo mapenzi?’’ kilihoji chanzo hicho
makini.
Baada ya paparazi wetu kuyanasa madai
hayo, Jumatano iliyopita alimtafuta Uwoya kwa njia ya simu ambapo
alipopewa taarifa hizo, alionesha kushtuka na kuchanganyikiwa mumewe
kuigiza filamu moja na Lucy, alikata simu kisha baadaye akampigia
paparazi yeye.
“Kuna wakati nilikuwa namtafuta Ndiku
sijui alipo kumbe alikuwa na Lucy, sawa lakini kama Lucy ameamua
kunifundisha mimi na sasa amemfundisha mume wangu sawa, tupo hapa!”
Paparazi wetu alihamishia majeshi kwa kumtwangia ‘mtuhumiwa’, Lucy ambaye alitiririka kama ifuatavyo:
“Nilijua Uwoya akisikia itakuwa ni
balaa maana siku za nyuma niliwahi kumshutumu kutoka na mzazi mwenzangu
(Patrick Mbasha) lakini mimi nipo tayari kwa lolote!”
Lucy Komba ndiye aliyemuingiza Uwoya
kwenye sanaa baada ya kumchezesha Filamu ya Yolanda ambayo ndiyo
iliyomtambulisha vyema staa huyo kisha kuliteka soko la sinema Bongo