Dar es Salaam. Idara ya Ujasusi ya Marekani imeweka bayana
kwamba inajitegemea kwa ulinzi katika ziara nzima ya Rais Barack Obama
kwa nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania, Afrika Kusini na Senegal.
Kwa mujibu wa taarifa ya idara hiyo, katika
kuhakikisha usalama wa kutosha wakati wa ziara ya Obama tayari maofisa
wao wameshakamilisha maandalizi ya kiusalama katika nchi zote
anazotarajiwa kutembelea.
Meli ya kivita kutua bandarini
Katika kuchukua hatua hizo, meli kubwa kabisa ya
kivita yenye hospitali maalum zipo tayari kwa ya kambi maalumu katika
bandari maalum za nchi atakazotembelea, kwa ajili ya kukabiliana na
dharura yoyote ya kiafya ya Obama na familia yake.
Ili kuwawezesha maofisa wa kijasusi wa Marekani,
ndege ya kijeshi ndiyo itakayobeba magari 56 zikiwemo limousine 14 na
magari matatu maalumu ya kubeba mizigo.
Malori hayo yatakuwa yakibeba vioo ambavyo ni
vizuizi maalumu vya risasi na milipuko kwa ajili ya kuongeza ulinzi
kwenye hoteli atakazolala yeye na familia yake.
Ndege za kivita kutawala anga
Ndege za kivita zitakuwa zikiruka kwa zamu wakati
wote muda wa sasa 24 kwa ajili ya kuhakikisha ulinzi katika sehemu
atakayokuwa Rais Obama na kudhibiti anga yote kwa wakati huo dhidi ya
ndege yoyote ngeni itakatosogea usawa wao.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mwananchi,
hakuna Maandalizi ya safari hiyo ambayo tayari yamekamilika
yanapolinganishwa na safari nyingine za aina hiyo zilizowahi kufanyika,
waraka maalumu kuhusu suala la usalama unaonesha kwamba kumekuwa na
juhudi za ziada zakuhakikisha ulinzi wa Amiri jeshi huyo Mkuu wa
Marekani akiwa nje ya nchi.
Kabla ya safari yake kwa nchi za Afrika, Obama
atatembelea Ireland na Ujerumani ikiwa ni sehemu ya kuongeza changamoto
inayokabili masuala ya usalama wake.
Lakini zaidi, safari ya Obama kwa nchi za Afrika
inadhaniwa kuwa inayolazimisha waandaaji kuwa na umakini wa hali ya juu
na kuifanya iwe aghali zaidi katika utawala wa Obama kuliko ziara katika
nchi za ulaya, kwa mujibu wa wataalamu wa mipango.
Familia ya rais huyo inatarajiwa kutembelea nchi
tatu za Afrika, ikiwemo Tanzania, Afrika Kusini na Senagal kuanzia Juni
26 hadi Julai 3 mwaka huu.
CHANZO NI MWANANCHI
CHANZO NI MWANANCHI