JAJI BOMAN ALISEMA "Najua bado ishu ya rasimu ya katiba mpya iko kwenye headlines
Tanzania ambapo time hii Mwanasheria mkuu mstaafu wa Serikali Jaji Mack
Bomani nae ametoa msimamo wake kuhusiana na muundo wa serikali na
kuamplfy kwamba ni vizuri katiba mpya iutambue muundo wa serikali tatu
kama ilivyopendekezwa na tume ya kuratibu maoni inayoongozwa na Jaji
Joseph Warioba.
Jaji Bomani anasema alipata fursa ya kutoa maoni yake na
kupendekeza muundo huo ambao utasaidia kutatua baadhi ya kero za
muungano ikiwemo mgawanyo wa mapato ambao kwa muda mrefu umekua
ukilalamikiwa.
Namkariri akisema “Wananchi wanatakiwa waachiwe waamue
wenyewe muundo gani wa Serikali wanautaka kwa kupiga kura badala ya
kuwaamulia, tuunde sasa Muungano au shirikisho la serikali tatu… moja
Zanzibar, Tanganyika na nyingine ya Muungano, wametoa sababu zao nyingi
na nzuri zipo kwenye hii rasimu, mimi nilifikisha maoni yangu mbele ya
tume hiyo kwa jambo ambalo nalielewa fika”
Jaji Bomani ametoa haya maoni siku moja baada ya CCM kusema
itatangaza msimamo wake baada ya kukusanya maoni ya Wanachama wake na
uamuzi utakaofikiwa.