NLC
Tuesday, April 1, 2014
KENYA BADO HALI YA AMANI NI MBAYA SANA;;BAADA YA WATU SITA NA WENGINE 25 KUJELUIWA KATIKA SHAMBULIO LA KIGAIDI JIJINI NAIROBI
Watu sita wamepoteza maisha na wengine 25 kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la kigaidi katika eneo la California mtaa wa Eastleig jijini Nairobi.
Kamanda wa Polisi mjini Nairobi Benson Kibue amesema kuwa milipuko miwili ilitokea wakati magaidi waliporusha milipuko katika migahawa miwili midogo.
Mlipuko wa tatu ulitokea katika kituo cha mabasi ya uchukuzi kilichopo karibu na zahanati ya mama na mtoto.
Miongoni mwa waliojeruhiwa walikuwa ni wanawake waliokuwa wanauza mboga na bidhaa nyingine za rejareja.
Kwa mujibu wa polisi watu waliouawa walikuwa wamekwama ndani ya mgahawa huo baada ya mlango wa kutoka nje kufungwa na washambulizi waliorusha bomu ndani.
Watu hao waliopoteza maisha walikuwa wameenda kununua chakula cha usiku.WATU SITA