NLC
Friday, March 21, 2014
NJAA YA DOGO JANJA YAFANYA HAMKUMBUKE MADEE NA BABA MZAZI WA DOGO JANJA AFUNGUKE ZAIDI
Alhamisi ya March 20 lilitoka tamko ni tamko la Dogo Janja kuhusu kuomba msamaha na kuhitaji kurudi kwenye kundi lake za zamani kama kutakuwa na huo uwezekano lakini kubwa zaidi aliloliomba ni msamaha kwa yale yaliyopita baina yake na Tip Top na aliyekuwa meneja wake Madee.
Stori hii ina pande nyingi sana ambazo zitazungumza kupitia hapa hapa na hapa tupo na baba yake mzazi Dogo Janja ambaye anaelezea jinsi alivyoyapokea maamuzi ya Dogo Janja>>’Dogo Janja alishakua mtu mzima na tayari nilishawahi kumwambia achague mahali atakapoona kuna manufaa kwake’
‘Akishafanya maamuzi yake huwa ananishirikisha kwenye kujadiliana kuwa nataka kufanya jambo hili au la,mimi tayari alishawahi kuniambia kuwa atafanya maamuzi baada ya kuona Mtanashati hakuna muelekeo wowote na hakuna anachopata ndipo akaniambia baba mimi mtu yoyote au kundi lolote nitakalokubaliana nalo basi nitafanya nao kazi’.