Van Persie akifunga mkwaju wa penati |
Kitu, Hulk akiifungia Zenit bao la kuongoza |
MASHAMBULIAJI
nyota wa Kiholanzi, Robin van Persie usiku wa kuamkia leo amefanikiwa
kuibeba Manchester United na kuivusha Roibo Fainali ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya bada ya kufunga hat trick wakiizamisha Olympiacos ya Ugiriki.
Manchester ambayo haikupewa nafasi kubwa
miongoni mwa timu za England, ilipata ushindi huo kwenye uwanja wake wa
nyumbani wa Old Trafford na kufuzu hatua hiyo kwa jumla ya mabao 3-2
kwani katika mechi ya kwanza walichezea kichapo cha mabao 2-0 ugenini.
Mfungaji Bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu
ya England, van Persie, alifunga utepe wa mabao kartika ya 25 kwa
mkwaju wa penati kabla ya kuongeza jingine sekunde chache kabla ya
mapumziko na kwa pasi ya Wayne Rooney na kuipeleka Mashetani Wekundu
mapumziko wakiwa mbele kwa 2-0.
Kipindi cha pili wageni wakilisaka bao la
kuwatibulia wenyeji, walishindwa kuhimili vishindo baada ya van 'Magoli'
kuongeza bao la tatu dakia saba baada ya kuanza kipindi cha pili.
Katika mechi nyingine iliyochezwa nchini
Ujerumani wanafainali wa mwaka jana wa michuano hiyo, Borussia Dotmund
walijikuta wakichezea kichapo nyumbani chja mabao 2-1 dhidi ya Zenit.
Wageni waliwashtukiza Dotmund kwa bao la
dakika 16 kupitia kwa Hulk kabla ya kuchomoa baadaye katika dakika ya 38
kupitia kwa Kehl aliyemalizia kazi ya Schmetzer na kufanya timu ziende
mapumziko zikiwa nguvu sawa hata jhivyo kipindi cha pili Zenith
waliandika bao la ushindi kupitia Rondon.
Hata hivyo ushindi huo ulishindwa kuibeba
Zenit kwa vile katika mechi ya kwanza nyumbani kwao walilala mabao 4-2,
hivyo kuwapisha Wajerumani kufuzu robo fainali kwa jumla ya mabao 5-4.
Ratiba ya hatua hiyo kwa timu nane
zilizofuzu inatarajiwa kutangazwa kesho, ingawa kuna hofu ya Chelsea
kuangukia mikononi mwa Barcelona, Bayern Munich au Atletico Madrid