KIWEWE NA MATUMAINI WAAMUA KUOKOKA...!!
MSANII wa Kundi la Ze Komedi, Robert Augustino ‘Kiwewe’ na mwenzake
Tumaini Martin ‘Matumaini’ wameamua kuacha anasa na kumrudia Mungu kwa
kuokoka.
Wakizungumza
na paparazi wetu kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema
kilichosababisha kuchukua uamuzi huo kwa wakati mmoja ni kutokana na
manzingira waliyolelewa tangu wakiwa wadogo, yaani kumjua Mungu.
“Niliamua
kufanya uamuzi sahihi ambao naamini utanibadilishia maisha yangu kwa
kiasi kikubwa, kwa kufuata mambo yanayompendeza Mungu na siyo starehe za
ujana,” alisema Kiwewe huku akiungwa mkono na Matumaini. Wakabainisha
kuwa wanasali kwa Mchungaji Josephat Gwajima.
Wasanii hao walisema,
ili kuhakikisha wanaungana na Mungu katika kila jambo, wameamua
kuanzisha kundi lao la muziki wa Injili, Comedians Gospel linaloundwa na
wao pamoja na Mkono.