TAMKO LA UMOJA WA WANAZUONI WA KIISLAMU TANZANIA KUHUSU TUKIO LA SHEIKH PONDA
Sisi, Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (Hay – atul Ulamaa),
tumepokea kwa masikitiko makubwa habari za kushambuliwa na kujeruhiwa
kwa silaha za moto, Sheikh Ponda Isa Ponda, huko Morogoro, Jumamosi
Agosti 10, 2013.
Hay-atul Ulamaa, imesitushwa na tukio hili
linalo uma na linaloumiza na kuleta mshtuko na fazaa katika jamii kama
ilivyoshtushwa na matukio mengine kama hili hapa nchini. Hili ni tukio
ambalo linaashiria kuwa walio litenda hawaitakii mema na amani nchi
yetu.
Tunalaani vikali kitendo
hicho na tunaitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchukua
hatua kali na za haraka dhidi ya wale wote walio husika katika tukio
hili lenye kuumiza nyoyo za wengi.
Aidha tunawasihi Waislamu na
jamii kwa ujumla kuwa watulivu, wenye subira na wenye kunyenyekea kwa
Mola wao katika jambo hili zito, wakati tunasubiri vyombo vya dola
vichukue hatua zinazo stahiki dhidi ya wahusika wa tukio hili.
Tunamuombea Sheikh Ponda Isa Ponda Allah Amponye haraka na Am,pe baraka katika umri wake. Amin