Tuesday, August 20, 2013

SERIKALI YAKANUSHA JUU YA MAMA SALMA KIKWETE KUWA SIO MNYARWANDA



Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye mtandao wa “twitter ”  na  wanyarwanda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal Havyarimana.

“Taarifa hizi haina ukweli wowote na zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Mrisho Kikwete,” amesema Mwambene na kufafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha umma wala siyo kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na ukweli wowote.


Madai  hayo  yaliandikwa  jana  na  mitandao  ya  Rwanda  wakidai  kuwa  mama  Salma  Kikwete  ni  Mnyarwanda  na  ni  binamu  wa  aliyekuwa  rais  wa  zamani  wa  Rwanda.