KATIBU wa Jumuiya ya Kiislamu nchini , Shekhe Ponda Issa Ponda
akihutubia kwenye Kongamano la Kiislamu lililofanyika kwenye uwanja wa
Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege , Kata ya Saba Saba , Manispaa ya
Morogoro, Jumamosi Agosti 10, 2013.
Shekhe Ponda Issa Ponda akihutubia kwenye Kongamano hilo.
Askari wa FFU wakijisongeza kati kati ya uwanja mara baada ya muda wa kongamano kumalizika.
Kikosi cha FFU uwanjani
Shekh Ponda akikaribishwa kwenye jukwaa kuu baada ya kuwasili kwenye
viwanja vya shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege , mjini Morogoro
Shekh Ponda akisalimiana na Mhadhiri wa Mihadhara nchini, Ustaadhi Abubakari
Shekh Ponda akisisistiza jambo mbele ya waumini wa Dini ya Kiislamu kwenye Kongamano , Augosti 10, mwaka huu mjini Morogoro
Shekh Ponda akiteta jambo na baadhi ya Viongozi wa umoja wa Wahadhiri wa Dini ya Kiislamu Mkoa wa Morogoro
Shekhe Ponda akiwa meza kuu kwenye kongamano hilo
Shekhe Ponda akiwa amezingirwa na waumini
Umati wa waumini wa Kiislamu wakimsikiliza Shekh Pond
Waumini wa Dini ya Kiislamu wa mjini Morogoro wakimsikiliza Shekh Ponda
Waumini wa Kiislamu wakitawanyika uwanjani baada ya muda wa kongamano kufikia tamati,
Na John Nditi, Morogoro.
KATIBU
wa Jumuiya ya Kiislamu nchini , Shekhe Ponda Issa Ponda, alijikuta
katika wakati mgumu baada ya kuumizwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni
risasi kwenye bega lake la kulia wakati akiekelea katika Msikiti wa
Mungu Mmoja Dini Moja wa Mjini Morogoro baada ya kumalizika kwa
kongamano ya Dini ya Kiislamu.
Mkasa
huyo ulitokea Jumamosi Augosti 10, mwaka huu majira ya saa 12: 15 za
jioni eneo la barabara ya Tumbaku karibu na Fire, mara baada ya kumaliza
kwa Kongamano la Kiislamu lililofanyika kwenye uwanja wa Shule ya
Msingi Kiwanja Cha Ndege, Kata ya Saba Saba , Manispaa ya Morogoro.
Shekhe
Ponda alishiriki katika Kongamano hilo lililoandaliwa na Umoja wa
Wahadhiri wa Dini ya Kiislamu Mkoani Morogoro na kufanyika siku ya Idd
Pili kuanza saa nane mchana hadi kumi na mbili jioni ya siku hiyo.
Kongamano
hilo lilipata baraka zote na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, ambalo
lilitoa masharti kadhaa ya kuzingatiwa na wazungumzaji ikiwa ni
kutokashifu dini nyingine wala viongozi wa serikali.
Sakata
la kutaka kutiwa mbaroni kwa Shekhe Ponda lilikuja baada ya yeye kudaiwa
kukiuka masharti ya Mahakama aliyopewa baada ya kuhukumiwa kifungo cha
mwaka mmoja nje wa kutakiwa asitende kosa lolote la jinai anapotumikia
adhabu hiyo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maadalizi ya Kongamano hilo, Ustaadhi Idd Msema, alidai
kuwa Shekhe Ponda baada ya kutoka ndani ya gari eneo la Uwanja wa Shule
ya Msingi Kiwanja Cha Ndege aliofika mita chache katika barabara ya
Tumbaku alitelemka na wakat akitaka kuingia garini ilifayuliwa risasi
iliyompiga begani.
Ustaadh
Msema alidai kuwa baada ya kupigwa risasi begani waumini waliokuwa
wameambatana naye walimchukua na kumpakiza kwenye Piki Piki hadi
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ili kupoatiwa matibabu.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti huyo, baada ya kufika hospitali, waliona
anacheleweshwa kpatiwa matibabu na ndipo walipoamua kumwondoa na
kumpekea kwenye Hospitali binafsi ambayo hakupenda kuitaja.
Akizungumzia
kwa kina hali ya Shekhe Ponda baada ya kujeruhiwa huko, alisema kuwa yu
hai licha ya kuumia vibaya begani na kwamba wanatarajia kumpekela eneo
jingine hususani Jijini Dar es Salaam kupata matibabu zaidi.
Alisema
viongozi wa Umoja huo hauwezi kuweka wazi sehemu anakotibiwa kwa kuwa
jambo hilo ni la kiusalama zaidi hasa wakati huu ambapo kumekuwa na
sinto fahamu.
Baadhi
ya walinzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro waliozungumza juu
ya tukio hilo , walikiri kuwa Shekhe Ponda aliletwa hapo kwa usafiri wa
Piki piki zikiambatana na nyingine zaidi ya 50 na kuishia getini.
Walisema
walimwingiza adi mapokezi na kwamba walipoona umati mkubwa upo getini
waliamua kutoa taarifa Polisi kuwa wamevamiwa na watu ambapo muda si
mrefu Polisi wa FFU waliwasili na gari lao Hospitalini hapo.
Hata
hivyo walinzi hao walisema, baada ya kuona Askari wamefika Hospitalini
hapo, baadhi ya wafuasi wa Shekhe Ponda waliamua kumyanyua na kumbeba
mabegani na kutoka naye mlango mwingine wakimlazimisha mlinzi
kuwafungulia mlango na baadaye wakatokomea naye kwa usafiri wa Pikipiki
kusikojulikana.
Kufikishwa
kwa Sheikh Ponda katika Hosipitali ya Rufaa kulithibishiwa pia na
Mwenyekiti huyo ambaye alidai kuwa waliamua kumwondoa baada ya
kuchekewa kupatiwa huduma.
Baada ya
tukio hilo, uvumi ulisambaa meneo mbalimbali nchini ukidai kuwa Shekhe
Ponda amepigwa risasi na Polisi na kufariki dunia. Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Morogoro, Feustine Shilongine akizungumza na Mwandishi wa Habari
hizi majira ya saa tatu usiku wa Augosti 10, baada ya kutokea kwa tukio
hilo, alisema kuwa hapakuwa na taarifa juu ya kutokea kifo cha Shekhe
Ponda.
“
Nimepingiwa simu zaidi ya 50 , zikiulizia jambo hili...kuwa Ponda
amefariki dunia ...Binafasi nami ninazisikia , ujumbe umesambazwa kwenye
simu za watu mbalimbali...tumezunguka kila mahali hakuna kifo wala
maiti yake ...na vijana wangu wanaendelea kulifuatilia suala hili”
alisema Kamanda huyo.
Juhudi
za kufuatilia sakata la uvumi kifo cha Shekhe Ponda uliendelea kufanyiwa
kazi na Ripota a wetu huyu na usiku wa saaa tano Mwenyekiti wa Kamati
huyo aliweka wazi kwa kusema kuwa Shekhe Ponda yu hai isipokuwa ameumia
vibaya sehemu ya bega.
“Nipo
katika eneo ambalo Shekhe Ponda anapatiwa matibabu...sehemu ambayo
hatuwezi kupataja kiusalama , isipo kuwa ameumia vibaya kwenye bega
lake. Lakini yu hai wala hajafa” alisema Msema. Polisi Mkoani hapa bado
haijatoa taarifa rasmi kuhusiana na sakata hilo, nasi twaendelea
kufuatulia kwa ukaribu.