PICHA ZA KWANZA TUKIO MOROGORO SHEIKH PONDA KUPIGWA RISASI
Leo
kwenye kongamano la kuita umoja wa waislam katika yanayo wakabili
waislam mkoani Morogoro..Kongamano lillienda vizuri likiwa limepambwa na
mashekh wakubwa wakubwa kama vile Riko,Mwaipopo,Kondo pamoja na shekh
Ponda.Shekh ponda alikuwa wa mwisho kutoa mawaidha na aliaga waislam ili
aweze kuelekea Msikiti wa Mungu mmoja hivyo waislam walitaka
kumsindikiza Shekh Ponda mpaka Msikiti wa Mungu mmoja.Maaskari
waliovalia nguo za fild force wakiwa kwenye defender waliingia na kuanza
kuifuata gari kwa nyuma.Waislam waliendelea kuizunguka gari ya Shekh
ponda ila maaskari walianza kupiga mabomu ya machozi ili kuwatawanya
wananchi kisha kuifukuza gari ya shekh Ponda