Hiki ndicho alichokifanya baada ya jina lake kutajwa kuwa ndiye anayetakiwa kutoka kwenye jumba la BBA.
Hatimaye mtanzania (Feza) aliyekua
amebaki kwenye jumba la BBA ametolewa. Huyu ni mtanzania wa pili
kutolewa baada ya Nando kutoka siku kadhaa zilizopita. Kwa sasa Tanzania
haina mshiriki ndani ya Jumba hilo.
Waliosimama ni washiriki watatu ambapo mmoja wao alitakiwa kutoka. Hapa wakisubiri Big Brother ataje nani wa kutoka
Pozi la Feza sekunde chache kabla hajatajwa kutoka
Pozi la Feza mara baada ya kutajwa kuwa anatakiwa kutoka
Feza akiagana na wenzake ambao wamebaki ndani ya jumba hilo
Akitoka nje na Bendera ya Tanzania, hapa akiwa amebakiwa na sekunde 10 za kuwepo ndani ya jumba hilo
Feza huyooo anapotelea, huku wenzake wakimuangalia kwa hamu