Thursday, August 15, 2013

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LIMETOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI ''PRESS RELEASE''


WILAYA YA  MBEYA MJINI – UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA [PANGA].

 MNAMO TAREHE 14.08.2013 MAJIRA YA SAA 16:50HRS HUKO AIRPORT - TANKINI JIJI NA MKOA WA MBEYA.  DANIEL S/O SONGELA, MIAKA 24, KYUSA, DEREVA WA PIKIPIKI @ BODABODA, MKAZI WA ZZK-MBALIZI,  ALINYANG’ANYWA PIKIPIKI YAKE T.691 CJF AINA YA  KINGLION  NA WATU WAWILI.  

MBINU NI KUKODIWA NA MTEJA  MMOJA KWA UJIRA WA TSHS 5,000/= KUTOKA MBALIZI HADI ENEO LA ESSO NA NJIANI WALIKUTANA NA MTU MWINGINE ALIYEVAA SARE ZA JWTZ AKIWA AMESHIKA PANGA HIVYO WALIFANIKIWA KUMPORA MHANGA PIKIPIKI HIYO. KUFUATIA TUKIO HILO JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WAENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA LILIFANYA MSAKO NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WAWILI 1. BARAKA S/O DAUDI, MIAKA 20, KYUSA, BIASHARA MKAZI WA MAMA JOHN NA 2.SHADRACK S/O ESSAU, MIAKA 21, BIASHARA , MKAZI WA MWAMBENE WAMEKAMATWA NA KUKIRI KUHUSIKA KATIKA MATUKIO YA  UPORAJI WA PIKIPIKI MAENEO MBALIMBALI. JUMLA YA PIKIPIKI NANE ZINAZODHANIWA KUWA MALI YA WIZI ZIMEKAMATWA KATIKA MSAKO HUKO TUKUYU WILAYA YA RUNGWE NA WATUHUMIWA SITA WAMEKAMATWA 1.SIMON S/O MWANYASI, MIAKA 35, KYUSA, MKULIMA 2.LWITIKO S/O HADSON, MIAKA 22, KYUSA, MKULIMA 3. OSFA S/O MWAMAKULA, MIAKA 38, KYUSA, MKULIMA 4.FESTO S/O GIDEON, MIAKA 35, KYUSA, MKULIMA 5.SOFIA D/O GIDEON, MIAKA 35, KYUSA, MKULIMA NA 6.NOEL S/O YESAYA, MIAKA 34, KYUSA, MKULIMA WOTE WAKAZI WA TUKUYU. 

TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII  KUACHA TABIA YA  KUJIPATIA KIPATO / MALI KWA NJIA YA  MKATO KWA TAMAA YA  UTAJIRI WA HARAKA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA  BADALA YAKE WAJISHUGHULISHE NA SHUGHULI HALALI ZA KUJIPATIA KIPATO. AIDHA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WALIOWAHI KUIBIWA AU KUPOTELEWA PIKIPIKI ZAO KUFIKA KITUO CHA POLISI KATI MBEYA KWA AJILI YA  UTAMBUZI WA MALI ZAO.

 

 

 

Imesainiwa na,

 [DIWANI ATHUMANI   - ACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.