Hakika kwa lililotokea mkoani mpanda basi si la kusahau kila rahisi,kwa historia kufutika kichwani mwangu na milele moyoni Mwangu.
Siku ya Jana wakati nimetokea jijini Tabora kwenye Fiesta 2013 baada ya kibarua ,hapa tena nakuja Mpanda nikiwa na crew yangu nzima. Majira ya saa 7 tulikuwa tumewasili uwanja wa ndege wa Binafsi Mkoani humu lakini baada ya Kuwasili na kutokeza tu nje,ghafla hali ya hewa ilibadilika kuwa ya Furaha na watu kujazana kwenye uzio wa uwanja wa ndege mdogo mkoani hapa. Kiukweli nilijua hali ile ingeishia pindi mimi nigehenda kuwasabahi lakini cha ajabu nilivyowasalimu ni mashabiki zangu wa kweli walikuwa wakiimba nyimbo zangu wakubwa kwa wadogo kiasi kwamba machozi ya furaha ndio yalitawala ndani yangu. Baada ya kumalizana nao ni zilifata kuzingirwa toka uwanja wa ndege hadi mjini,watu wa mpanda
Namshukuru Mungu na daima ntamshukuru Mungu kwa kuzidi kunipa kibali chake mimi na crew yaangu nzima kukubalika na kuzidi kufanya vizuri.....Nawapenda mashabiki zangu sana,kwenye kila nyanja ya Tanzania na Afrika nzima.
Baada ya Kupumzika Nimeamua kukuwekea pich hizi Asubuhi ya leo kuona tukio zima lilivyojiri so unaweza pata taswira ya kile nilichokuwa nakuambia hapo Mwanzo. |