Msichana mrembo kutoka Iran amejikuta akikosa nafasi ya uongozi katika halmashauri ya jiji lake kwa kuambiwa kuwa yeye ni mzuri sana hivyo amepitiliza sifa za nafasi hiyo.
Nina Siahkali Moradi (27), alikuwa miongoni mwa wagombea katika uchaguzi wa halmashauri ya jiji la Qazvin nchini Iran, ambapo baada ya kura kuhesabiwa alikamata nafasi ya 14.
Lakini hata hivyo wiki moja baadaye kura zake zilifutwa na kiongozi wa halmashauri ya jiji hilo kwa maneno ya kejeli akimwambia “We don’t want a catwalk model on the council,”
Katika uchaguzi huo Nina alipata kura 10,000 na kumfanya akamate nafasi ya 14 kati ya 163, lakini wapinzani wake katika uchaguzi huo walilalamika kuwa Moradi alipigiwa kura kwasababu ni mzuri sana anavutia, pia mdogo.
Kwa mujibu wa The Independent, baraza huchukua washindi 13 wa juu na mgombea anayeshika nafasi ya 14 huwekwa kama ‘reserve’.