Saturday, July 6, 2013

SASA SIRI NZITO YAIBUKA HUKO SOUTH AFRIKA KUHUSIANA NA HALI YA MZEE MANDELA


Nelson Mandela ameendelea kuwekwa hai kwa msaada wa mashine za kumsaidia kupumua na  'anakaribia kifo,' nyaraka za mahakama zimefichua.

Afya ya rais huyo wa zamani ni 'yenye hatari kubwa,' kwa mujibu wa nyaraka zilizowasilishwa mahakamani kwenye kesi ambayo imepelekea mabaki ya miili ya watoto wake watatu kuzikwa upya Alhamisi kwenye makaburi yao ya awali.
 
Nyaraka za mahakama za Juni 26 zilisema: "Matarajio hayo ya kukaribia kifo chake yanaegemea katika uhalisia na uthabiti,' zilisema nyaraka hizo za mahakama.
 

Mandela, ambaye alilazwa hospitali Juni 8, ameendelea kuwa mahututi lakini hali inayoimarika, kwa mujibu wa Ofisi ya Rais Jacob Zuma, ambaye alimtembelea kiongozi huyo wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi Alhamisi.


Ikulu ya Afrika Kusini imekanusha kwamba Mandela yuko kwenye 'hali ya kulala tu', na kurejea taarifa zake zilizopita kwamba kiongozi huyo mpendwa yuko mahututi lakini katika hali inayoimarika.


Ikulu hiyo ilitoa taarifa 'inayofafanua' hali ya Mandela, imeripotiwa.

Walisema: "Tunathibitisha taarifa zetu  zilizotolewa awali ... baada ya Rais Jacob Zuma kumtembelea Madiba hospitalini."


Mandela yuko chini ya uangalizi wa karibu wa timu ya wauguzi, ikulu hiyo ilisema, masaa kadhaa baada ya ripoti hizo za kusisimua za mahakama kufichuka.


Nyaraka hizo zilisomeka: Wanasema hali ya rais wa kwanza mweusi wa nchi hiyo ni 'yenye hatari kubwa'. "Matarajio ya kukaribia kifo chake yanaegemea katika uhalisia na uthabiti,'  ziliongeza. 


Nyaraka hizo za kisheria zinahusiana na mapambano makali ya kisheria yenye chuki kati ya makundi yanayopingana kwenye familia kuhusu wapi Mandela atakapozikwa.

Baada ya kumchunguza wiki iliyopita, madaktari waliandika: 
 "Yuko kwenye hali ya kudumu ya kulala tu na anasaidiwa kupumua na mashine ya kuokoa maisha."


Kitabibu, hii inamaanisha hajitambui na yuko kwenye hali katikati ya kuzimia kwa muda mrefu na kifo.

"Kwa kifupi ameshakufa," alisema Charlene Smith, mwandika wasifu wa Mandele aliyethibitishwa.

Taarifa hizo zimekuja huku mabaki ya watoto watatu wa mzee huyo mwenye miaka 94 yakiwa yamezikwa upya kwenye makaburi yao ya awali kufuatia amri ya mahamaka kuirejesha miili hiyo baada ya mjukuu wake, Mandla kuwa ameihamisha.