Friday, July 12, 2013

IRENE UWOYA YA KUMTOKEA PUANI,, AFUNGUKA BAADA YA MAMBO YAKE NA DIAMOND

clip_image002Kufuatia kuripotiwa kwa habari "kali" sana iliyopewa kichwa "DIAMOND AFICHUA KISA CHA KULALA NA UWOYA!" leo kuhusu mwanadada Irene uwoya na Msanii wa kizazi kipya Diamond platnumz leo na mtandao wa Global publishers, hatimaye Irene Uwoya alichukua dakika kadhaa kuandika hichi alichokiandika hapa chini....
 “Kuna saa najiuliza kwanin ukimwamin mtu ndio anageuka...kwanin ukiwa muwaz watu wanakuchukulia vbaya? Leo nimeumia sanaaa kuliko skuzote...sijaamini mtu niliye mwamini kumuona kama rafiki yangu anaweza kuongea shit kuhusu mim...au najiuliza siruhusiwi kuwa na rafik wa kiume? Lakin sa nyingine nakaa chin nasema God ...u know me better”
MCHUNGUZI wa mambo anasema maneno hayo ni kutokana na kile alichokiona kama ni usaliti wa namna fulani toka kwa rafiki yake wa karibu (Jina kapuni) kuamua kumuanika hadharani mdada huyo wa bongo movies.