Saturday, July 6, 2013

EXILE ZAZIDI HUKO MAVYUONI NI AIBU SANA SASA HAPA TANZANIA

MWANACHUO WA MWAKA WA KWANZA ALAANI KITENDO CHA KUPIGWA "EXILE" NA MADENTI WENZIE

Vitendo  vya  wanafunzi  kupigana  exile( kumpisha room ili angonoke na mpenzi wake)   vimekuwa  vikishika  kasi  ya  ajabu  katika  hosteli  za  wanafunzi  wa  vyuo  vikuu  mbalimbali ambao  kwao  limekuwa  ni  jambo  la  kawaida...!!

Hali  imekuwa  ni tofauti  kidogo  kwa  mwanafunzi  wa  chuo kimoja  hapa  nchini  ambaye  yuko  mwaka  wa  kwanza na anategemea kuingia mwaka wa pili.


Akiongea  na  mtandao  huu  kwa  sharti  la  kutotajwa  jina , mwanafunzi  huyo  amefunguka  na kudai  kuwa  Exile  imemuathiri  sana  kisaikolojia.Imemfanya  aishi  kama  mtumwa  huku  taaluma  yake  ikiyumba  kwa  kasi.

Hili  ni   simulizi  la  mwanafunzi  huyo:
 
"Maisha ya shule yana changamoto  nyingi sana.Kwa  mtu  yeyote  ambaye  ni  mcha  mungu  ni  lazima  itamuwia  vigumu  sana  kukabiliana  na  hali hii.

"Nasema  hivi  kwa  sababu  ndani  ya  hosteli  huwa  tunaishi  watu   tofauti  wenye malezi  tofauti.Kasheshe  ni  kwetu  sisi  first  year...

"Mazingira  kwetu  ni  mageni  na  ndani  ya  hosteli  tunaishi  na  mabraza  wa  miaka  ya  juu  wenye  wapenzi  wao  hapo hapo chuoni ambao  huwaleta  vyumbani   na  wakati mwngine  hulala  nao.

"Wanapokuja  na  wapenzi  wao  vyumbani  ni  lazima  uwapishe  wafanye  mambo  yao.Na  ukiwapisha  maana  yake  utoke  kwa  zaidi  ya  masaa  matatu  mpaka   matano

"Ndani  ya  chumba  changu  tulikuwa  tunaishi  watatu, mmoja  mwaka  wa  pili, mwingine  wa  tatu  na  mimi  mwaka wa kwanza.Wote  hao  walikuwa  na  wapenzi  wao  hapo hapo  chuoni.

"Siku  zote  za  wikiendi  walikuwa  wamezigawana.Mmmoja  ilikuwa  ni  jumamosi  na  mwingine  jumapili.Yaani  kwa  kifupi  ni  kwamba  sikuwa  na  uhuru wa  kukaa  chumbani   siku za wikiendi  na  wakati  mwingine  hata  siku  za  wiki.

"Nimeamua  niwe  muwazi  maana hali  hii  imekuwa  ni  kero  kwangu   na  imekuwa  ikiniathiri  sana  kisaikilojia  na  kusababisha  taaluma  yangu  iyumbe  nikilinganisha  na  nilipokuwa  naanza.

"Naomba  nitoe  ombi  kwa  wanafunzi wenzangu.Sote  tuko  vyuoni  kutafuta  maisha  na  zile  hosteli  tunazilipia  kwa  gharama  sawa.Kwa  nini  umsumbue  mwenzako  wakati  gesti  zipo?..Yangu  ni  hayo  tu"