Hii ilikuwa siku ya jana baada ya kupata futari na ndugu,jamaa
na marafiki na watu wasiojiweza
Presenter wa kipindi cha Take One Zamaradi ambae nae alikuwa
mmoja wa wageni waalikwa aliamua
kubadilisha mazingira na kuamua kunifanyia Interview mimi
pamoja na familia yangu
juu ya mfungo huu wa ramadhani na Jinsi tunavyokabiria na mambo
mbalimbali ya kidunia ndani ya mwezi huu...
Aliweza pia kuongea na Mama yangu mzazi Bi Sandrah,Cuzin
Brother Rommy Jones,Dada zangu Esmah & Darlenee .....
Kuzungumzia mambo ya ndani ya kifamilia na n.k
Unaweza ukacheki picha kadhaa za nyuma ya pazia za Interview hiyo ya Take one special
ndani ya mwezi wa ramadhani iliyofanyika nyumbani kwangu sinza,bila kusahau
utaona kabisa kipindi kizima ndani ya TAKE ONE kwenye luninga yako kupitia
Channel ya CLOUDS TV...kila Jumanne saa 9:30 usiku...USIKOSEEEE..!!
|