Sunday, July 14, 2013

BREAKIN NEWZZZZZ


Bus la kampuni ya Najma linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Nachingwea, limepata ajali kwenye daraja la Mkapa, Ikwiriri baada ya kugonga pikipiki na kusababisha vifo vya watu wawili papohapo. Chanzo cha ajali hiyo ni moshi mkali uliotanda kwenye eneo la ajali kutokana na moto uliokuwa unaunguza majani yaliyopo pembezoni mwa barabara ya kusini mara baada ya kumaliza daraja la Mkapa. Basi hilo lilikuwa linatokea Nachingwea kwenda Dar es Salaam. Watu waliofariki ni wale waliokuwa kwenye pikipiki. Ajali hiyo imetokea majira ya saa 6:40 mchana. Hata hivyo gari hilo halikupinduka isipokuwa imeharibika vibaya sehemu ya mbele. Baada ya ajali hiyo, dereva alisogeza gari kwenye kituo cha polisi cha Ikwiriri na baada ya kutoa maelezo, polisi wameenda eneo la tukio kuchukua maiti. Mtoa habari hii ni miongoni mwa watu waliokuwa abiria kwenye basi hilo. Namba ya gari ni T 599 CBL aina ya YUTONG.