Baada
Waziri wa Ujenzi, Pombe Magufuli kutoa maagizo kwa wenye majengo yaliyo
pembezoni mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi, kubomoa wenyewe majengo
yao ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo, kuonekana yakisua sua,
hatimaye leo ameanza rasmi kazi ya kubomoa kwa Greda katika majengo ya
wale walioonekana kukaidi agizo hilo. Katika kutekeleza agizo hilo zoezi
hilo limeanzia kwenye Jengo la Business Park (Green Acres) lililopo
eneo la Victoria ambapo hadi hivi sasa zoezi hilo bado linaendelea pande
hizo chini ya usimamizi ya Askari wakishirikiana na Watu wanaoonekna
kuwa ni wa Majembe.
Tayari
ukuta ukiwa umeshashushwa chini wa upande wa barabarani. huku baadhi ya
watu wanaofanya shughuli zao katika jengo hilo wakihaha kuhamisha
baadhi ya vifaa.