SHIRIKA
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), imepanga kuwafikia wajasiriamali
wapya zaidi ya milioni 22 walio katika sekta isiyo rasmi. Hayo yamesemwa
na Meneja wa Mafao wa shirika hilo, James Oigo wakati wa Semina ya kukuza
mitaji kwa njia ya ubia katika sekta zisizo za kibenki iliyofanyika
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kuwashirikisha wadau
mbalimbali. Semina hiyo ilidhaminiwa na NSSF, TPSF.
Akichangia
mada katika semina hiyo, Oigo alisema kuwa NSSF inatoa mafao ya muda
mrefu na muda mfupi yakiwemo mafao ya ya matibabu.
'Watu wengi wanatumia gharama kubwa kwenye matibabu na kuwaongezea umaskini kwa sababu ya gharama kubwa za matibabu".
“Mafao yetu
yamejikita kusaidia wateja wa sekta binafsi na wa serikali, lakini pia hata
wale wanaofanya kazi kwa kujitegemea kama atakuwa mwanachama wetu atapatiwa fao
hilo kama wengine tena katika hospitali atakayochagua yeye mwenyewe katika zile
ambazo tumeingia nazo mkataba na kupewa fao hilo”. alisema.
Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSS) inatoa Mafao ya Pensheni ya uzee,
Mafao ya pensheni ya ulemavu, Mafao ya pensheni urithi, Mafao ya
mazishi, Mafao ya uzazi, Mafao ya kuumia kazini na magonjwa yatokanayo
na kazi na Mafao ya matibabu.
Meneja wa Mafao wa Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii (NSSF), James Oigo akitoa mada kuhusu wafanyabiashara wadogowadogo,
kujua maana ya kuwepo kwenye hifadhi ya jamii kwa ajili ya maisha yao ya
baadae, katika semina ya kukuza mitaji
kwa njia ya ubia katika sekta zisizo za kibenki iliyofanyika jijini Dar es
Salaam hivi karibuni. Katikati ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi
Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi. Semina hiyo ilidhaminiwa na NSSF.