Thursday, October 17, 2013

RAISI WA ZANZIBAR Dr SHEIN AWATOA HOFU WANANCHI NA WAGENI JUU YA UVAMIZI WA MAGAIDI NCHINI HUMO PIA ULINZI UMEWEKWA KILA SEHEMU

Znz hali shwari oct 16 2013Ripoti ambayo imetolewa na Farouq Karim wa ITV October 16 2013 kuhusu hali ya usalama Zanzibar, inasema Rais wa Zanzibar Dr. Ally Mohamed Shein amewahakikishia Wananchi na wageni kutokua na hofu kwa vile Serikali yake kupitia vyombo vya ulinzi na usalama vitahakikisha amani inalindwa.
Dr Shein kwenye hotuba yake ya baraza la Idd Tunguu Zanzibar amesema Zanzibar iko kwenye amani kote Unguja na Pemba lakini bado wako wakorofi wachache ambao ndio wanavuruga na kuleta hofu kwa Wananchi na wageni.
Namkariri Dr. Shein akisema ‘nawahakikishia Wananchi na wageni wetu kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinafanya kazi nzuri ya kusimamia ulinzi na usalama wa nchi lakini vinategemea sana ushirikiano kutoka kwetu’