Ni
siku zisizozidi 5 toka bodi ya Utalii Tanzania kutangaza kwamba
Tanzania kwa mwaka 2012 peke yake Utalii umeingiza shilingi Trilioni
2.69 kwenye pato la taifa ikiwa ni ongezeko la asilimi 24 ikilinganishwa
na mwaka 2011 na kwamba Watalii wanaotembelea Tanzania kutoka nje ya
nchi wamekua wakiongezeka kila mwaka kutoka Watalii laki nane na elfu
67,994 mwaka 2011 mpaka milioni moja na elfu sabini na saba 58 mwaka
2012.Tanzania ina mbuga nzuri sana za Wanyama na sehemu nyingine nzuri za kutengeneza pesa zinazotokana na Utalii na ninaamini kama zikitangazwa kwa nguvu na kufika kunakotakiwa hata hiyo Trilioni 2.6 kwa mwaka itakua ndogo, yani mkwanja utaingia mrefu zaidi.
Nimefurahi
kwenda Cinema na kutazama movie mpya ya Baggage claim na kukutana na
sehemu ya movie hiyo ambayo jamaa alikua anaongea na mrembo akitaka
azunguke nae sehemu mbalimbali duniani ikiwemo kuitembelea mbuga ya
wanyama ya Serengeti.Nilijua hii ishu ingekua kubwa kwangu tu ila kiukweli watu niliokua natazama nao movie nao walifurahi tena wengine wengi tu kupiga makofi ya midadi nikiwemo mimi… ni movie ambayo ndani yake kuna mastaa kama Trey Songz, Paula Patton na Lauren London.
Hii sio mara ya kwanza kwa Tanzania kuingia kwenye headlines kwa kutajwa na mastaa wa majuu, nakumbuka kwa harakaharaka miongoni mwa waliowahi kuitaja ni pamoja na mwigizaji wa movie za Action Steven Seagal alieitaja Dar es salaam na mtangazaji Oprah ambae alikuja Tanzania siku kadhaa zilizopita.
